jinai za israel

IQNA

IQNA: Baada ya kufariki kwa idadi ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza kutokana na baridi kali, Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombzoi wa Palestina, Hamas, imeonya kuhusu kuzidi kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika eneo hilo ambalo liko chini ya mzingiro wa utawala katili wa Israel.
Habari ID: 3481801    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA – Tangu kuanza kwa vita vya kikatili vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, angalau Wapalestina 21 wamefariki katika eneo hilo kutokana na baridi kali na ukosefu wa vifaa vya kujihifadhi na kupashia joto, hali ambayo imesababisha na hatua ya Israel kuzuia misaada kufika eneo hilo.
Habari ID: 3481797    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Wapigania haki za Wapalestina wamezindua kampeni mahsusi ya vyombo vya habari yenye lengo la kuwakomboa wafungwa walioko katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel, wakisisitiza kuwa mshikamano wa kimataifa na uelewa mpana ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha uhuru wao.
Habari ID: 3481783    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina ameonya kwamba vizuizi vipya vilivyowekwa na Israel vinakwamisha kabisa usambazaji wa misaada huko Gaza, vinazidisha hali ya njaa na kuweka “mfano hatari” kwa shughuli za kibinadamu duniani kote.
Habari ID: 3481749    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/01

IQNA- Utawala haramu wa Israel unaendelea kulaaniwa vikali  baada ya kushambulia kikatili sherehe ya harusi Gaza huku shirika mashuhuri la haki za kiraia za Waislamu nchini Marekani likitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.
Habari ID: 3481694    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/21

IQNA-Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (Hamas) imelaani vikali mauaji ya makusudi na mateso ya Wapalestina walioko katika magereza ya kuogofya ya utawala haramu wa Israel, ikiyataja kama “uhalifu kamili wa kivita” na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti.
Habari ID: 3481575    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/27

IQNA – Dar al-Ifta ya Misri imetoa fatwa mpya ya kidini inayoruhusu raia kuelekeza mali ya zakat kusaidia mahitaji ya msingi ya watu waliokoseshwa makazi huko Gaza.
Habari ID: 3481373    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

IQNA-Vita vya Ghaza na jinai nyingine zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel zimekabiliwa na msururu wa mashinikizo ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ambayo yameufanya utawala huo ghasibu kuwa taifa linalochukiwa na kukataliwa duniani.
Habari ID: 3481334    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/05

IQNA – Hatua ya utawala wa Israeli kuzuia meli za Msafara wa Kimataifa wa Sumud imezua shutuma kali kutoka kwa serikali na mashirika ya kimataifa kote duniani.
Habari ID: 3481315    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/02

IQNA – Harakati za mapambano ya ukombozi wa Wapalestina, Hamas na Jihad ya Kiislamu, zimetoa matamko ya kulaani hatua ya Marekani kutumia kura ya turufu au veto kuzuia kupitishwa kwa rasimu ya azimio la kusitisha vita Gaza, wakisema kuwa hatua hiyo inachochea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3481253    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/19

IQNA – Akielezea unyama unaoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina, Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesisitiza haja ya kukatisha mahusiano yote na Israel.
Habari ID: 3481187    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/05

IQNA – Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Yemen walifanya maandamano makubwa siku ya Ijumaa kulaani uhalifu wa Israeli dhidi ya Wapalestina na kitendo cha hivi karibuni cha kuchomwa motot nakala ya Qur’an Tukufu nchini Marekani.
Habari ID: 3481160    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/30

IQNA-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali Alhamisi katika Makao Makuu ya Unmoja wa Mataifa jijini New York akilihimiza Baraza la Usalama na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuwalinda raia wa Gaza wanaokabiliwa na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3481151    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/29

IQNA- Mamlaka ya anga ya Israel imesitisha safari zote za ndege za kuwasili na kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion na kusema kuwa kituo hicho kitaendelea kufungwa "kwa muda usiojulikana" baada ya Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen kufanya shambulio la kombora, kulipiza kisasi vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea vya utawala wa Tel Aviv dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Habari ID: 3480912    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/07

IQNA-Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimeanza kutekeleza wimbi la mashambulizi ya makombora dhidi ya utawala waKizayuni Israel, ili kulipiza kisasi kufuatia hujuma za utawala huo wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Iran.
Habari ID: 3480831    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/14

IQNA – Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ameelezea kwa uchungu hali ya mateso ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akisema ni jambo linalomuumiza sana kila anapofikiria yanayoendelea katika eneo hilo.
Habari ID: 3480823    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/11

IQNA – Wapalestina kote Ukanda wa Gaza wameswali Swala ya Idul Adha juu ya magofu ya misikiti iliyoharibiwa na vita vya kinyama vya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo.
Habari ID: 3480799    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/07

IQNA-Ofisi ya Habari ya Serikali katika Gaza imetangaza kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya mauaji mapya ya halaiki dhidi ya raia wa Kipalestina katika maeneo ya usambazaji wa misaada ya kibinadamu, ambayo yanajulikana kama “mitego ya kifo”, ambapo watu wasiopungua 30 wameuawa shahidi na zaidi ya 120 kujeruhiwa.
Habari ID: 3480773    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/01

IQNA-Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amezitaka nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kutenga tone tu la fedha zilizotajwa katika ‘makubaliano makubwa’ kati yao na Rais wa Marekani, Donald Trump, ili kusaidia wakimbizi wa Kipalestina wanaopambana kuendelea kuishi katika ardhi zao ambazo Israel imezikalia kwa mabavu na pia wale wanaoishi katika nchi jirani.
Habari ID: 3480762    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30

IQNA-Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) limeripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 97,000 wamehamishwa Gaza katika kipindi cha siku nne pekee, huku mashambulizi ya Israeli yakizidi kuwa makali katika eneo hilo lenye mateso.
Habari ID: 3480710    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/20